• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpira wa Wavu, Rwanda: Hatimaye Timu ya Busagara yawasajili wachezaji wa kigeni

    (GMT+08:00) 2018-01-04 10:34:57
    Mabingwa watetezi wa ligi ya mpira wa wavu nchini Rwanda, imewasajili wachezaji machachari wa kigeni Ongom Ivan Bob kutoka timu ya Sport-S ya Uganda pamoja na mchezaji nyota kutoka Kenya Nikolas Matui wa timu ya Water Club.

    Wawili hao wanatarajiwa kujiunga na timu hiyo mapema mwezi ujao baada ya kukamilisha taratibu za usajili.

    Gisagara wameendelea kujifua kwa ajili ya msimu mpya wa ligi hiyo huku wakinunua wachezaji wapya.

    Wachezaji wengine waliosajiliwa na timu hiyo ni Vincent Dusabimana na Eugene Tuyishimire, wote kutoka chuo kikuu cha Kibungo.

    Wengine ni Yves Niyonkuru and Peter Bigirimana wote kutoka timu ya REG, pamoja na Nelson Murangwa alisajiliwa kutoka Tricolorul LMV ya Romania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako