• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Watalii waongezeka Kenya

  (GMT+08:00) 2018-01-04 18:38:56

  Idadi ya watalii nchini Kenya imekua kwa asilimia 7.8 ndani ya kipindi cha miezi 10 kufikia mwezi Oktoba mwaka jana.

  Ukuaji huo umeshuhudiwa licha ya kuwepo na hali ya kisiasa mwaka 2017.

  Taakwimu za halmashauri ya utali nchini humo KTB zinaonyesha kuwa watalii wa kigeni walifikia 786,765 kati ya Januari na Oktoba mwaka 2017 ikilinganishwa na watalii 729,682 kipindi sawa na hicho mwaka 2016.

  Watalii wengi kulingana na KTB walitokea Merekani na China, nchi mbili hizo zikiwa na ongezeko la asilimia 16.

  Hata hivyo watalii kutoka India walipungua kwa asilimia 3.7 huku wale kutoka Uingereza wakiongezeka kwa asilimia 7.5.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako