• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Wakulima wa mahindi Kenya wadai malipo

    (GMT+08:00) 2018-01-04 18:39:27

    Wakulima wa mahindi nchini Kenya wameitaka serikali kuwalipa shilingi milioni 45 za mahindi waliowasilisha kwa bodi ya kitaifa ya nafaka nchini humi mwezi Desemba.

    Zaidi ya wakulima 100 wameandama wakitaka kulipwa kwa kuuza magunia 70,000 kwa bodi hiyo.

    Wamesema bodi hiyo imelipa shilingi milioni 30 tu nab ado haijatoa tamko kuhusu pesa zilizosalia.

    Makubaliano kati ya bodi hiyo na wakulima yanaonyesha kuwa wangelipwa pindi tu baada ya kuwasilisha mahindi.

    Lakini sasa wakulima wanalalama kwamba hawawezi kulipia watoto wao karo kutokana na ucheleweshaji huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako