• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Afrika kusini yaanzisha uchunguzi kuhusu ajali ya treni

    (GMT+08:00) 2018-01-05 08:39:45

    Wizara ya uchukuzi ya Afrika kusini imeanzisha uchunguzi kuhusu ajali ya treni iliyotokea Alhamisi na kusababisha vifo vya watu 18 na wengine 239 kujeruhiwa. Taarifa iliyotolewa na waziri wa uchukuzi wa Afrika kusini Bw. Joe Maswanganyi, inasema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa ajali ya treni kuacha reli ilisababishwa na lori lililojaribu kuvuka reli hiyo saa tatu jana asubuhi wakati treni hiyo inapita, treni hiyo ya umeme iliwaka moto baada ya kugonga lori na kusababisha vifo na majeruhi. Waziri Maswanganyi alitembelea eneo la ajali na kutoa salamu za rambirambi kwa familia za wahanga katika ajali hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako