• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika zatakiwa kupambana na ufisadi kwa kufuata ajenda ya Umoja wa Afrika

    (GMT+08:00) 2018-01-05 08:47:52

    Wataalamu na watunga sera wa nchi za Afrika, wamezitaka nchi za Afrika kupambana na ufisadi kwa kufuata ajenda ya umoja wa Afrika, ili kutimiza maendeleo ya Afrika.

    Mwito huo umetolewa siku chache kabla ya kufanyika kwa mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika, unaotarajiwa kufanyika mjini Addis Ababa kuanzia tarehe 22 hadi tarehe 29, chini ya kauli mbiu ya "kupambana na ufisadi kwa ajili ya maendeleo endelevu".

    Kauli mbiu hiyo imewavutia wataalamu na watunga sera, kutokana na mchango inaoweza kutoa kwenye ongezeko la jumla la uchumi wa Afrika na maendeleo.

    Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Mahamat amesema kupambana na ufisadi ni sehemu muhimu ya juhudi za kuleta maendeleo, na kuondoa hali ya kutokuwa na usawa barani Afrika. Hata hivyo amesema katika miaka mitano iliyopita Afrika imepata maendeleo makubwa kwenye mapambano dhidi ya ufisadi, lakini changamoto bado zipo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako