• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia yakataa pendekezo la Marekani kuitisha Mkutano wa dharura wa UN kuhusu Iran

    (GMT+08:00) 2018-01-05 09:26:44

    Russia inaona kuwa pendekezo la Marekani kuitisha mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu maandamano yaliyotokea hivi karibuni nchini Iran, litakuwa na athari mbaya.

    Shirika la habari la Sputnik la Russia likimkariri naibu waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergei Ryabkov, limesema Baraza la Usalama lina wajibu wa kulinda amani na usalama duniani, na mambo ya ndani ya Iran hayahusiani na jukumu lake. Pia amesema Russia itaonesha msimamo unaoendana na sheria za kimataifa.

    Mapema wiki hii, balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Bibi Nikki Haley, alisema Marekani ilikuwa inajaribu kuitisha mkutano wa dharura kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa na Baraza la haki za binadamu mjini Geneva.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako