• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yamwita balozi wake nchini Misri kwa ajili ya majadiliano

    (GMT+08:00) 2018-01-05 09:28:02

    Shirika la habari la Sudan SUNA likimkariri msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo Bw. Gariballah al-Khider, limesema serikali ya Sudan imeamua kumwita nyumbani balozi wake nchini Misri kwa ajili ya kufanya majadiliano.

    Uhusiano kati ya Misri na Sudan umekuwa katika hali ya wasiwasi katika miaka kadhaa iliyopita kutokana na masuala mbalimbali.

    Mwezi Mei mwaka 2017, rais Omar al-Bashir wa Sudan aliishutumu Misri kwa kutoa msaada wa kijeshi kwa waasi nchini mwake, kauli ambayo ilipingwa na viongozi wa Misri.

    Nchi hizo mbili pia zina mgogoro wa ardhi katika sehemu za mpaka za Halayeb na Shalateen, ambazo sasa zinadhibitiwa na Misri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako