• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Botswana yakaribisha marufuku ya China dhidi ya biashara ya pembe za ndovu

    (GMT+08:00) 2018-01-05 09:28:32

    Mamlaka ya wanyamapori na wataalamu nchini Botswana wamekaribisha marufuku iliyotolewa na China dhidi ya biashara ya pembe ya ndovu wakiona hii ni hatua muhimu ya kupunguza kuuawa kwa wanyama walio hatarini.

    Waziri wa mazingira, maliasili na utalii ya Botswana Bw. Tshekedi Khama amesema, hatua hiyo imetoa matumaini kwa mustakabali wa tembo nchini Botswana, na nchi nyingine barani Afrika.

    China imepiga marufuku biashara ya pembe za ndovu na bidhaa zake, marufuku hiyo imeanza kutekelezwa mwanzoni mwa mwaka huu.

    Ofisa wa shirika la ulinzi wa tembo "Elephants Scents" nchini Botswana amesema marufuku hiyo tayari imefanikiwa kupunguza kwa asilimia 80 ya pembe za ndovu zinazoingizwa kwa magendo nchini China, na asilimia 65 kwa bei ya pembe za ndovu nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako