• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampuni ya sayansi na teknolojia ya safari ya anga ya juu ya China kurusha vyombo 35 vya anga ya juu mwaka huu

  (GMT+08:00) 2018-01-05 16:41:00

  Mwaka huu Kampuni ya sayansi na teknolojia ya safari ya anga ya juu ya China itarusha vyombo 35 vya anga ya juu kwa mara 35 vikiwemo roketi ya Changzheng-5, chombo cha uchunguzi wa mwezi cha Chang'e-4, na mtandao wa satilaiti za Beidou, ambavyo ni vingi zaidi kuliko miaka iliyopita.

  Kiongozi husika wa kampuni hiyo amesema katika mwaka huu kampuni hiyo itainua uwezo wa uvumbuzi, kuhimiza miradi mikubwa, kutoa maoni ya uongozi kuhusu safari za anga ya juu za kibiashara, kupanua soko kwa njia yenye unyumbufu, kufanya ushirikiano kati ya sekta za jeshi na teknolojia katika soko la kimataifa, na kuhimiza mauzo ya bidhaa za safari ya anga ya juu zenye teknolojia ya juu katika nchi za nje.

  Kabla ya hapo, kampuni hiyo ilitoa mpango wa utengenezaji wa vyombo vya anga ya juu hadi mwaka 2025, ikiamua kuunga mkono utafiti na uzalishaji kwa teknolojia ya habari na akili bandia, kutekeleza mradi wa kuboresha mfumo wa injini za roketi zinazotumia nishati ya majimaji, ili kukidhi mahitaji ya urushaji wa vyombo vya anga ya juu ya mwaka mzima.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako