• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Serikali ya Iraq lamuua kiongozi muhimu wa kundi la IS

    (GMT+08:00) 2018-01-05 18:10:37

    Mkuu wa kamati ya usalama ya mkoa wa Diyala, nchini Iraq Bw. Sadiq al-Husseini amesema, jeshi la nchi hiyo limemuua kiongozi muhimu wa kundi la IS mkoani Diyala, mashariki mwa nchi hiyo.

    Bw. al-Husseini amesema, jeshi hilo limefanya operesheni katika eneo la milima la Himreen, na kumuua mpiganaji anayeitwa "Abu Ayed". Idara ya ujasusi ya serikali ya Iraq imemfuatilia kwa muda mrefu na kugundua kuwa ni kiongozi muhimu wa kundi la IS.

    Ofisa huyo pia amesema, jeshi hilo limeondoka katika miji na wilaya muhimu za mkoa huo na kukabidhi shughuli za ulinzi wa usalama kwa polisi wa huko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako