• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yatoa wito wa waislamu kushikamana kupambana na sera ya Marekani ya kuleta mgawanyiko

    (GMT+08:00) 2018-01-08 08:57:14

    Iran imezihimiza nchi za kiislamu kushirikiana kwa karibu zaidi ili kupambana kwa pamoja na sera ya Marekani inayolenga kuleta mgawanyiko miongoni mwao. Katibu wa Baraza kuu la usalama la Iran Bw Ali Shamkhani amesema hayo alipokutana na mshauri wa usalama wa Pakistan Bw. Nasser Khan Janjua, ambaye nchi yake imekosolewa na rais Donald Trump wa Marekani. Bw. Shamkhani pia amesisitiza kuwa hawataruhusu nchi za nje kuhujumu uhusiano kati ya nchi hizo mbili kupitia kupeleka silaha na kuajiri magaidi kuchochea machafuko kwenye mipaka yao. Kwa upande wake, Bw. Janjua amezihimiza nchi za kiislamu kuwa na tahadhari dhidi ya njama za kigeni zinazolenga kuchochea mgawanyiko kati yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako