• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Algeria na Tunisia zajadili ushirikiano kuhusu kupambana na ugaidi

    (GMT+08:00) 2018-01-08 09:34:10

    Algeria na Tunisia zimejadili njia za kuimarisha ushirikiano wa kiusalama kati yao, ikiwa ni sehemu ya ajenda ya ziara ya waziri wa mambo ya ndani ya Tunisia Bw. Lotfi Brahem nchini Algeria.

    Baada ya kukutana na mwenzake wa Algeria Bw. Noureddine Bedoui, Bw. Brahem amesema lengo la ziara yake ni kutathmini na kujenga ushirikiano wa kiusalama kutokana na uzoefu wa awali kwenye huduma za usalama kwa ajili ya nchi hizo mbili na wananchi wao.

    Kwa upande wake Bw. Bedoui amesema, mkutano huo ni fursa kujadili uhusiano wa pande mbili na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano na uratibu kati ya mashirika ya usalama ya nchi hizo mbili ili kulinda nchi zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako