• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwenyekiti wa chama cha ANC aahidi kutekeleza sera ya mageuzi ya ardhi

    (GMT+08:00) 2018-01-08 09:38:20

    Mwenyekiti mpya wa chama cha African National Congress (ANC) cha Afrika Kusini Bw Cyril Ramaphosa, ameahidi kuwa atatekeleza sera ya mageuzi ya ardhi. Amesema chama cha ANC kinaendelea kutaifisha ardhi bila ya fidia.

    Sera ya mageuzi ya ardhi ilikuwa imewezekana mwaka 1994, wakati sera ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini ilipokomeshwa, lakini hakuna maendeleo makubwa yaliyofikiwa katika kugawanya upya ardhi kwa watu weusi, ambao ardhi yao ilitwaliwa kutokana na sera hiyo ya ubaguzi wa rangi.

    Bw.Ramaphosa amesema kugawanya upya ardhi kwa wananchi wa Afrika Kusini ni njia ya kutatua suala la ardhi nchini humo. Mageuzi ya ardhi yatatafuta ufumbuzi mwafaka usioharibu uchumi na sekta ya kilimo, na kutoathiri usalama wa chakula. Ameongeza kuwa licha ya kuhimiza utatuzi wa suala la ardhi, mageuzi hayo ya ardhi pia yanatakiwa kuhimiza ongezeko la uchumi na uzalishaji wa kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako