• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kusini na Korea Kaskazini kufanya mkutano wa ngazi ya juu

    (GMT+08:00) 2018-01-08 18:46:06
    Korea Kusini na Korea Kaskazini zitajadili masuala kuhusu uhusiano wao, yakiwemo ushirikiano wa kijeshi na haki za binadamu ambayo yalipendekezwa na Korea Kusini mwaka uliopita, taarifa hii ni kwa mujibu wa wizara ya muungano ya Korea Kusini.

    Msemaji wa Wizara hiyo ya masuala ya muungano Baek Tae-Hyun amewaambia waandishi wa habari kuwa, mkutano huo kwanza utajadili kuhusu suala la DPRK kushiriki katika mashindano ya Olimpiki ya majira ya baridi PyeongChang na olimpiki ya watu wenye ulemavu.

    Uhusiano wa kiwenzi wa kuendeleza ukaribu wa nchi hizo mbili ni mada itakayokuwa msingi wa majadiliano hayo, mfano suala la dharura lililopendekezwa na Korea Kusini mwezi Julai mwaka jana.

    Watu kutoka nchi hizo mbili walizuiliwa kutembeleana au kuwasiliana tangu vita vya peninsula ya Korea vya mwaka 1950-53, vilivyoisha kwa mapatano ya kusimamisha vita kwa muda, na si kwa njia ya amani. Na mpaka sasa Peninsula inabaki kuwa na katika hali ya vita.

    Mkutano huo wa majadiliano yenye hisia kali kati ya pande hizo mbili unakuja baada ya hutoba ya mwaka mpya ya kiongozi wa DPRK Kim Jong Un ambaye alisema nchi yake ingependa kushiriki mashindano ya olimpiki ya majira ya baridi ambayo yatafanyika nchini Korea Kusini, na siku moja baada ya hotuba hiyo Korea Kusini wakatangaza kufanya mkutano wa majadiliano na Korea Kaskazini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako