• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan yatambua shambulizi la mjini Kabul kama uhalifu wa kivita

    (GMT+08:00) 2018-01-08 20:20:37

    Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, UNAMA imeonya kuwa, shambulizi la hivi karibuni la kujitoa mhanga mjini Kabul, linaweza kutambuliwa kama tukio la uhalifu wa kivita.

    Tume hiyo imetoa uchunguzi iliofanya juu ya shambulizi Januari 4 mjini Kabul, ambapo kundi la IS limejitangaza kuwa ndilo lililohusika, na shambulizi hilo limedaiwa kuua watu wasiopungua 13, wakiwemo askari wa vikosi vya uliniz, na kujeruhi wengine 19, muda mfupi baada ya polisi wa kuzuia maandamano walipofika kunyamazisha fujo zilizodumu saa kadhaa kati ya walinzi na wafanyabiashara wa maduka.

    12 kati ya watu 13 waliouawa ni maafisa wa polisi , waliokuwa wanatekeleza wajibu wao wa kisheria wa kurejesha utuluvu na usalama kwa raia.

    UNAMA imesisitiza kuwa, kila polisi wa Afghanistan anatambuliwa kama raia, isipokuwa tu pale atakapokuwa anashiriki katika matukio ya kupambana na uhalifu. Askari waliouawa katika shambulizi hilo hawakuwa miongoni mwa waliokuwa wanapambana kwa silaha. . Raia hawapaswi kujeruhiwa kamwe katika mashambulizi yoyote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako