• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan kusini yasema aliyekuwa kiongozi wa jeshi ameasi

    (GMT+08:00) 2018-01-09 08:43:57

    Sudan Kusini imesema aliyekuwa kiongozi wa jeshi la nchi hiyo Bw. Paul Malong Awan ameiasi serikali ya nchi hiyo. Msemaji wa rais wa nchi hiyo Bw. Ateny Wek Ateny amesema mnadhimu mkuu huyo wa zamani wa jeshi la Sudan Kusini SPLA ameamuru wafuasi wake kushambulia taasisi za kiserikali kwenye sehemu mbalimbali nchini humo, na kwamba mapambano yaliyoibuka wiki iliyopita karibu na mji mkuu Juba pia yaliamuriwa na Bw. Malong. Mashirika ya kibinadamu pia yamemshutumu Bw. Malong na wapiganaji wake kwa kufanya ukatili dhidi ya raia wa kawaida nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako