• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Angola yatahadharisha dhidi ya ugaidi wa kimataifa, na kuweka sera ya kubana matumizi kifedha ili kufufua uchumi

    (GMT+08:00) 2018-01-09 09:48:14

    Rais Joao Lourenco wa Angola ameutaja ugaidi wa kimataifa kuwa tishio kuu, huku akibainisha sera ya kubana matumizi ya kifedha kuwa njia ya kufufua uchumi wa Angola.

    Rais huyo amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari katika ikulu ya nchi hiyo. Mahojiano yake yamefuatilia maendeleo aliyopata katika siku 100 za mwanzo tangu aingie madarakani, ikiwemo kuendeleza mageuzi ya kiuchumi, na kumfuta kazi Bi Isabel dos Santos, binti wa rais wa zamani Bw. Jose Eduardo dos Santos, kutoka wadhifa wa mkuu wa Shirika la mafuta la nchi hiyo.

    Amesema sera ya kubana matumizi ya kifedha ni njia ya kutatua msukosuko wa kiuchumi na kifedha unaoikabili nchi hiyo, na kuimarisha uchumi wa kitaifa. Pia amesisitiza kuwa Angola inakusudia kubinafsisha makampuni yote ya umma yasiyo na faida.

    Rais Lourenco ameongeza kwamba Angola inajitahidi kuzuia kuathiriwa na ugaidi wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako