• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Klabu zaanza kujiandaa kwa ajili ya msimu wa mwaka 2018

  (GMT+08:00) 2018-01-09 09:51:46

  Wakati msimu wa ligi kuu ya mpira wa kikapu nchini Uganda wa mwaka 2017 ukielekea ukingoni, tayari vilabu vimeanza kujiandaa na msimu mpya wa mwaka 2018 ikiwemo usajili wa majina mapya pamoja na marekebisho ya miakataba kwa baadhi ya wachezaji.

  Timu ya Power Basketball Club ndiyo imeonekana kuongoza katika harakati hizo, ikiwemo usajili wa nyota anayeng'ara Steven Wundi iliyomsajili kutoka UCU Canons.

  Wundi anachukua nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Burundi Willy Njimbere ambaye mabingwa hao mara tano wa ligi kuu walimwachia aondoke.

  Kuhusu maendeleo ya ligi hiyo ambayo sasa ipo katika hatua ya nusu fainali Power Basketball wamejikuta wakifungwa mechi tatu mfululizo na bingwa mtetezi City Oilers.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako