• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misri kufanya uchaguzi wa urais mwezi Machi

    (GMT+08:00) 2018-01-09 10:23:06

    Tume ya uchaguzi ya Misri imetangaza kuwa, uchaguzi wa urais nchini humo utafanyika tarehe 26 hadi 28 mwezi Machi mwaka huu, na matokeo ya mwisho yatatangazwa tarehe 1, mwezi Mei.

    Mwezi Novemba mwaka jana rais Sisi alisema uchaguzi mkuu utafanyika mwezi Machi na Aprili kama ilivyopangwa, na kusisitiza kuwa hatajaribu kubadilisha ukomo wa kikatiba wa mihula miwili ya urais.

    Rais Sisi ametangaza rasmi kugombea urais, na anatarajiwa kupata ushindi kwenye uchaguzi huo, kutokana na kutokuwepo kwa mpinzani mwenye nguvu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako