• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yachukua hatua kuimarisha usalama mijini

  (GMT+08:00) 2018-01-09 18:26:59

  Ili kuimarisha uhakikisho wa usalama, na kuzuia ajali mijini, ofisi ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na ofisi ya baraza la serikali la China hivi karibuni zimetoa "maoni kuhusu kusukuma mbele maendeleo ya usalama mijini", na kufafanua mpango husika na hatua za kuutekeleza.

  Takwimu zinaonesha kuwa, hadi sasa zaidi ya nusu ya wachina wanaishi mijini. Wakati idadi ya watu mijini inaongezeka kwa haraka, mfumo wa kuendelea miji umezidi kuwa na utatanishi kutokana na mabadiliko makubwa ya njia ya maendeleo, muundo wa uzalishaji na mpangilio wa maeneo, huku matishio dhidi ya usalama yakiongezeka siku hadi siku. Katika miaka ya hivi karibuni, ajali kubwa za uzalishaji zimetokea katika baadhi ya miji hata majiji, na kusababisha hasara kubwa ya mali na hata maisha ya watu. Mtaalamu wa taasisi ya utafiti wa usanifu na mipango miji ya China Bw. Xu Chaoping anasema,

  "Kutokana na maendeleo na kupanuka kwa haraka kwa miji, mahitaji ya kupita kiasi kwa maliasili yamesababisha maafa ya aina mpya. Kwa mfano kuvuta maji chini ya ardhi kwa wingi kupita kiasi kumesababisha maporomoko, na kuharibu mimea milimani kumesababisha mmomonyoko wa udongo. Aidha, tumegundua kuwa katika baadhi ya mitaa mikongwe mijini, hata hakuna njia ya kupita magari ya kuzima moto."

  "Maoni kuhusu kusukuma mbele maendeleo ya usalama mijini" yametoa mpango na hatua za kuutekeleza, na kuiagiza miji mbalimbali kujenga jukwaa la kusimamia habari kuhusu matishio dhidi ya usalama, na kuweka rangi nyekudu, rangi yaachungwa, rangi ya njano na rangi ya buluu kwenye ramani za miji ili kuonesha viwango vya matishio. Maoni hayo pia yanaitaka miji yote iandae vitabu kuhusu matishio dhidi ya usalama, na kutoa kwa umma kila baada ya wakati. Profesa Zhang Zhixin wa Chuo Kikuu cha Uchumi na Biashara cha Beijing anasema,

  "Wakazi wa miji wamezoea kupata habari mbalimbali kupitia simu za mkono. Tukiwa na ramani zenye rangi za kuonesha viwango vya matishio, si kama tu wafanyakazi wa serikali wataweza kuchukua hatua za kukabiliana na matishio kwa haraka, bali pia wakazi wa kawaida watafahamu vizuri hali ilivyo ya matishio."

  Maoni hayo pia yameagiza kukamilisha orodha ya maelekezo kwa serikali kununua huduma za kuhakikisha usalama wa uzalishaji, na kutekeleza hatua za kuhakikisha usalama wa uzalishaji kwa nguvu kubwa, ili kukinga ajali. Bw. Zhang amesema maagizo hayo yataongeza ufanisi wa serikali katika kusimamia usalama wa miji na kupunguza gharama.

  "Maoni hayo yametekeleza mawazo ya kuhimiza serikali kununua huduma za kijamii, ili kushirikisha mashirika yasiyo ya kiserikali kujiunga na juhudi za kuhakikisha usalama mijini. Hali ambayo itatusaidia kuongeza ufanisi wa kuzuia matishio."

  Maoni hayo pia yameahidi kuongeza bajeti kwa uhakikisho wa usalama mijini, kueneza teknolojia za kisasa, na kuongeza uwezo wa mifumo ya kujiendesha ya kuchunguza na kukinga matishio.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako