• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Korea Kaskazini kutuma ujumbe wa ngazi ya juu kushiriki kwenye michezo ya Olimpiki

  (GMT+08:00) 2018-01-09 19:25:15

  Korea Kaskazini imekubali kutuma ujumbe wa ngazi ya juu wa wachezaji na ujumbe wa kamati ya Olimpiki ya nchi hiyo kushiriki kwenye michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya PyeongChang.

  Akizungumza baada ya kumaliza kwa ajenda zote za mkutano wa ngazi ya juu kati ya Korea Kusini na Korea Kaskazini, naibu waziri wa mawasiliano wa Korea Kusini anayeshughulikia masuala ya peninsula ya Korea Bw. Chun Hae-sung amesema, nchi yake imependekeza ushirikiano na Korea Kaskazini wakati wa ufunguzi wa michezo hiyo.

  Pia Korea Kusini imependekeza kufanya hafla ya kuungana tena kwa familia katika sikukuu ya Spring, na kufanya mkutano wa mashirika ya Msalaba Mwekundu na ya kijeshi ili kuzuia mapambano

  Kwa upande wake, Korea Kaskazini imekubali kutuma ujumbe wa Kamati ya Taifa ya Olimpiki, wachezaji, washangiliaji, timu ya sanaa, timu ya maonyesho ya utamaduni wa Taekwondo, watalii na waandishi wa habari kushiriki kwenye michezo hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako