• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Serikali ya Tanzania yasema uchumi umekua

    (GMT+08:00) 2018-01-09 19:53:25

    Serikali ya Tanzania imesema, hali ya uchumi wa nchi inaendelea kuwa imara kwa kiasi cha kuridhisha taasisi mbalimbali za kimataifa. Kwa mwaka huu wa fedha, unatarajiwa kukua kwa asilimia 6.5 hadi 7.0 na kuifanya Tanzania kuendelea kuwa kati ya nchi tano bora za Afrika.

    Mkurugenzi Mkuu, Idara ya Habari (MAELEZO) ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi alisema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa miradi.

    Alisema Ripoti ya Shirika la Fedha Duniani (IMF), Benki ya Dunia (WB) na Taasisi ya Goldman Sachs ya Marekani zimetabiri kuwa wakati uchumi wa dunia utakua kwa wastani wa asilimia 3.0 hadi 4.0, ukuaji wa uchumi wa Tanzania unatajwa kuendelea kuwa kati ya nchi tano bora za Afrika ukitarajiwa kukua kwa asilimia 6.5 hadi 7.0 katika mwaka 2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako