• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfumko wa bei nchini Tanzania kwa mwezi Desemba mwaka jana ulipungua hadi asilimia 4

    (GMT+08:00) 2018-01-10 09:24:24

    Idara ya takwimu ya taifa ta Tanzania NBS imesema kutokana na kupungua kwa bei ya vyakula, kiwango cha mfumko wa bei nchini Tanzania kimepungua hadi asilimia 4 ya mwezi Desemba mwaka jana, ikilinganishwa na asilimia 4.4 ya mwezi Novemba.

    Taarifa iliyotolewa na idara hiyo imesema kupungua huko kumeonyesha kwamba bei ya vyakula katika mwezi Desemba ilishuka ikilinganishwa na bei ya mwezi Novemba. Na ongezeko la mfumko wa bei kwa mwezi limefikia asilimia 0.2 mwezi Desemba, likipungua kutoka asilimia 0.5 la mwezi Novemba.

    Taarifa pia imesema mfumko kwa mwaka kwenye matumizi ya vyakula imepungua hadi kufikia asilimia 6.7 ya mwezi Desemba, ikilinganishwa na asilimia 7.9 ya mwezi Novemba. Na kiasi cha mfumko wa bei kwenye bidhaa zisizo za vyakula katika mwezi Desemba imepungua kidogo hadi asilimia 2.8, kutoka asilimia 2.9 ya mwezi Novemba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako