• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Upinzani Zimbabwe wasema kiongozi wao Bw Tsvangirai hajajiondoa

    (GMT+08:00) 2018-01-10 09:24:31

    Chama cha upinzani cha Zimbabwe kimetoa taarifa ikisema, kiongozi wake Bw. Morgan Tsvangirai hatajiondoa, kinyume cha ripoti zilizotolewa hivi karibuni na vyombo vya habari.

    Hoja hiyo imetolewa baada ya Bw. Tsvangirai kuelezwa kwenye taarifa ya mwaka mpya kuwa anafikiria kukabidhi uongozi kwa kizazi kijacho.

    Msemaji wa chama hicho Bw. Obert Gutu ametoa taarifa ikisema, tofauti na ripoti zilizotolewa hivi karibuni na vyombo vya habari kwamba Bw. Tsvangirai ataachia uongozi wa chama hicho, ukweli ni kwamba Bw. Tsvangirai ataendelea kuwa kiongozi wa chama cha MDC na atakuwa mgombea wa chama hicho katika uchaguzi wa urais utakaofanyika mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako