• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misri yawa mzalishaji mkubwa wa tatu wa fiberglass duniani kwa msaada wa China

    (GMT+08:00) 2018-01-10 09:41:22

    Waziri wa biashara na viwanda wa Misri Bw. Tarek Kabil, amesema Misri imekuwa mzalishaji mkubwa wa tatu wa fiberglass duniani baada ya Marekani na China, kwa msaada wa uwekezaji wa kampuni kubwa ya China.

    Kwenye taarifa Bw. Kabil amesema kila mwaka Misri inazalisha tani laki 2 za fiberglass, na asilimia 99 zinasafirishwa kwenda katika nchi nyingine.

    Bw. Kabil amesema hayo baada ya kukutana na mkurugenzi wa kampuni ya Jushi ya China nchini Misri Bw. Zhang Wenchao, ambapo wamejadili hali ya sasa na mustakabali wa uwekezaji wa kampuni hiyo kwenye soko la fiberglass nchini Misri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako