• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wapiganaji zaidi ya 107 wa kundi la Boko Haram wauawa katika operesheni ya jeshi la Nigeria

  (GMT+08:00) 2018-01-10 09:52:08

  Wapiganaji zaidi ya 107 wa kundi la Boko Haram wameuawa katika operesheni ya jeshi la Nigeria, miongoni mwao zaidi ya 50 wameuawa karibu na ziwa Chad na wengine zaidi ya 57 wameuawa kwenye eneo la Metele la jimbo la Borno nchini Nigeria.

  Msemaji wa jeshi la Nigeria Bw. Sani Usman ametoa taarifa akisema lengo la operesheni hiyo ni kuondoa wapiganaji wa kundi hilo waliosalia katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

  Msemaji huyo ameongeza kwamba askari wanne wa jeshi la Nigeria na raia mmoja anayejitolea pia wameuawa kwenye operesheni hiyo, baada ya deraya walilokuwa wakisafiria kugongwa na gari lenye mabomu ya kienyeji lililoendeshwa na wapiganaji wa kundi hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako