• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yajitahidi kuboresha sifa za bidhaa

  (GMT+08:00) 2018-01-10 18:17:45

  Mkutano wa mwaka 2018 wa kazi za usimamizi na ukaguzi wa sifa za bidhaa na ukaguzi wa maradhi umefanyika jana mjini Beijing. Takwimu zilizotolewa kwenye mkutano huo zinaonesha kuwa, kiwango cha bidhaa zilizofikia vigezo katika ukaguzi kimezidi asilimia 90 katika miaka minne mfululizo. Baadaye China itaendelea na juhudi za kuboresha sifa ya bidhaa, ili kujijenga kuwa nchi yenye bidhaa bora zaidi.

  Katika miaka mitano iliyopita, China imepiga hatua kubwa katika kutekeleza sera za mageuzi na ufunguaji mlango, na kujenga ujamaa wa mambo ya kisasa. Kwenye mkutano uliofanyika jana, mkuu wa idara kuu ya ukaguzi wa ubora wa bidhaa ya China Bw. Zhi Shuping amesema, katika miaka kadhaa iliyopita, sifa ya bidhaa nchini China imeboreshwa, huku watu wakizingatia zaidi ubora wa bidhaa siku hadi siku. Anasema,

  "Kuanzia mwaka 2014, kiwango cha bidhaa zilizokidhi vigezo vya ubora wa bidhaakwenye ukaguzi wetu kimezidi asilimia 90 kwa miaka minne mfululizo. Kati ya bidhaa hizo, magari, mitambo maalumu, dawa za kikemikali na vifaa vyenye usahihi mkubwa zilizofikia vigezo zimezidi asilimia 95. Aidha ubora wa bidhaa zinazouzwa kwa njia ya mtandao wa Internet pia umeinuka na kuridhisha wateja."

  Katika sekta ya usalama wa taifa, idara za ukaguzi wa sifa za bidhaa zimejenga mfumo kamili wa kuhakikisha usalama wa viumbe nchini China, na viumbe vyenye hatari kutoka nchi za nje vilivyozuiliwa kuingia China vimeongezeka zaidi ya asilimia 33 kwa mwaka. Aidha, idara hizo zimeimarisha nguvu ya usimamizi wa chakula kutoka nchi za nje, na kujenga kimsingi utaratibu wa tahadhari na kukabiliana na matishio ya usalama wa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje. China pia imetuma vikundi vya madaktari wanaoshughulikia maradhi ya kuambukiza katika nchi nyingine, ili kuhakikisha usalama wa China. Bw. Zhi anasema,

  "Tumefanya kazi kwa makini katika miaka mitano iliyopita. Kwa mfano baada ya kutokea maradhi ya kuambukiza katika nchi nyingine zikiwemo homa ya Ebola, homa ya manjano na maambukizi ya virusi vya Zika, kwa mara ya kwanza tulituma vikundi vya madaktari, ili kuzuia maradhi hayo yasiingie nchini China."

  Bw. Zhi amesema China pia imeongeza ushirikiano wa kimataifa katika kazi za ukaguzi wa sifa za bidhaa, haswa katika utekelezaji wa pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

  Mwaka jana, idara kuu ya ukaguzi wa ubora wa bidhaa ya China imechukulia kuboresha sifa za bidhaa kuwa ni kazi ya kwanza, na kufanya ukaguzi dhidi ya aina 198 za bidhaa muhimu. Mkurugenzi wa ofisi ya idara hiyo Bw. Lin Wei anasema,

  "Idara kuu ya ukaguzi wa ubora wa bidhaa zimepanga mwaka huu kuwa ni mwaka wa kuboresha sifa ya bidhaa, na itajitahidi kuinua viwango vya nyanja tano zikiwemo sifa za jumla za bidhaa, uhakikisho wa usalama, na miundombinu husika. Tutafanya kazi hizo kwa kushirikiana na idara nyingine, ili kupata ufanisi wa haraka."

  Mkuu wa idara kuu ya ukaguzi wa sifa za bidhaa ya China Zhi Shuping amesema, kwa mujibu wa mpango uliowekwa na China, hadi kufikia mwaka 2035, China itakuwa nchi yenye sifa nzuri ya bidhaa, na kuwa nchi yenye sifa nzuri zaidi ya bidhaa duniani ifikapo mwaka 2050, ili kuweka msingi wa sifa ya bidhaa kwa ajili ya ujenzi wa nchi yenye nguvu zaidi ya kijamaa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako