• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Mataifa wasema robo tatu za wakimbizi wa Syria nchini Lebanon wanaishi chini ya mstari wa umaskini

  (GMT+08:00) 2018-01-10 19:21:28

  Ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imesema, robo tatu za wakimbizi wa Syria waliokimbilia Lebanon wanaishi chini ya mstari wa umaskini na wahitaji msaada wa dharura wa kimataifa.

  Ripoti hiyo imesema, katika wakimbizi zaidi ya milioni moja ya Syria waliokimbilia Lebanon, asilimia 58 kati yao, kila mmoja anaishi kwa dola za Maerkani 2.87 kwa siku.

  Msemaji wa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, Bw. William Spindler amesema, hivi sasa, wakimbizi hao wanatumia dola za Marekani 98 kwa mwezi, ambapo dola 44 inatumika katika vyakula. Asilimia 90 ya wakimbizi hao wanakopa pesa kwa ajili ya kununua vyakula, matibabu na kulipa kodi.

  Habari zinasema, hadi mwanzo wa mwezi wa Desemba, mwaka jana, asilimia 36 tu ya fedha za misaada kwa wakimbizi hao zimelipwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako