• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu zaidi ya 2,800 nchini Zambia waambukizwa ugonjwa wa kipindupindu

  (GMT+08:00) 2018-01-10 19:30:01

  Waziri wa afya wa Zambia Bw. Chitalu Chilufya amesema watu 2,802 nchini humo wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu, ambapo watu 64 wamefariki kutokana na ugonjwa huo, na wengine 218 wanapatiwa matibabu.

  Bw. Chilufya amesema, kuanzia leo, wizara yake itaanza kutoa chanjo ya kukinga kipindupindu kwa watu milioni 2 katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka.

  Rais Edgar Lungu wa Zambia jana alitembea kituo cha matibabu ya kipindupindu kwenye uwanja wa michezo wa mashujaa wa taifa huko Lusaka, na kusema serikali itachukua hatua za kutoa maji ya kunywa na vifaa vya kuondoa takataka, ili kudhibiti kipindupindu kwa mwafaka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako