• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaongeza juhudi kupambana na matishio ya kiafya ya kimazingira

    (GMT+08:00) 2018-01-11 09:11:45

    Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP na Shirika la Afya Duniani WHO wameanzisha ushirikiano kuhusu kuharakisha hatua za kukabiliana na matishio ya kiafya yanayotokana na hali ya kimazingira, ambayo yanasababisha vifo vya watu milioni 12.6 kila mwaka.

    Mashirika hayo yamesaini makubaliano mjini Nairobi, Kenya, ili kuanzisha operesheni ya pamoja ya kupambana na uchafuzi wa hewa, mabadiliko ya hali ya hewa, na usugu wa vijidudu dhidi ya dawa, na kuimarisha uratibu kuhusu udhibiti wa takataka na kemikali, ubora wa maji, chakula na lishe.

    Hayo ni makubaliano muhimu kuhusu masuala ya mazingira na afya kufikiwa katika zaidi ya miaka 15 iliyopita. Mashirika hayo mawili yataweka mipango ya pamoja ya kazi, na kuandaa Mkutano wa ngazi ya juu kutathmini maendeleo yatakayopatikana na kutoa mapendekezo kwa ushirikiano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako