• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Trump asema Marekani inaweza "kurudi kwenye" Mkataba wa Paris

    (GMT+08:00) 2018-01-11 09:12:13

    Rais Donald Trump wa Marekani amesema Marekani inaweza "kufikiria" kurudi kwenye Mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, ambao Marekani ilitangaza mwaka jana kuwa itajitoa.

    Rais Trump amesema hayo katika mazungumzo kati yake na waziri mkuu wa Norway Bw. Erna Solberg, lakini amesisitiza kuwa Mkataba wa Paris uliosainiwa mwaka 2015 kwa lengo la kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa njia ya kupunguza ongezeko la joto duniani, ulikuwa "mpango mbaya" na sio wa "haki" kwa Marekani.

    Ameongeza kuwa mkataba huo utapunguza uwezo wa ushindani wa Marekani, na hataruhusu hali hiyo kutokea.

    Kauli hiyo ya Trump inaonesha kuwa msimamo wake hauna mabadiliko tangu mwaka uliopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako