• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Benki ya dunia yatahadharisha kuhusu hatari kwenye ongezeko la uchumi mashariki ya kati na Afrika Kaskazini kwa mwaka huu

  (GMT+08:00) 2018-01-11 09:27:32

  Benki ya dunia imesema ongezeko la uchumi katika eneo la mashariki ya kazi na Afrika Kaskazini kwa mwaka huu litaendelea kutatizwa na siasa za kikanda.

  Makadirio ya hatari za kiuchumi, zikiwa tofauti kwa waagizaji wa mafuta na wauzaji wa mafuta, yote yanaonyesha mwelekeo wa kupungua. Hatari za siasa za kijiografia za kanda hiyo bado ziko juu, na zimetatizwa na mivutano ya kidiplomasia.

  Ripoti iliyotolewa na benki ya dunia inasema tangu mwezi Juni mwaka jana wakati Bahrain, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu na Misri zilipokatisha uhusiano wa kibalozi na Qatar, usafiri wa majini na anga kutoka nchi hizo kwenda Qatar umezuiwa. Na licha ya kuwa hali ya kiuchumi kwenye nchi zinazoagiza mafuta inaonekana kuboreka, mustakabali wao uko hatarini kutokana na kuenea kwa madhara ya migogoro ya kivita ya Libya, Syria na Yemen.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako