• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Novak Djokovic asema atashiriki michuano ya Australia

  (GMT+08:00) 2018-01-11 09:28:47
  Baada ya kuwaweka mashabiki wake njia panda, hatimaye mchezaji namba 14 kwa viwango vya ubora dunia Novak Djokovic wa Serbia amesema atashiriki mashindano makubwa ya Australia yanayoanza wiki ijayo mjini Melbourne.

  Djokovic ambaye alishuka kwa viwango vya ubora kutokana na kutoshiriki kwa muda mrefu mashindano kufuatia majeruhi kwa mara ya mwisho alionekana katika mashindano ya Wimbledon.

  Endapo Nyota huyo atashiriki na kutwaa taji hilo basi ataweka rekodi kwa atakuwa ameshinda mara nyingi zaidi, kwa kufikisha mataji 7, ambapo mpaka sasa ameshinda mara 6 ambayo ni sawa na mkongwe mwingine Roy Emerson wa Australia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako