• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • CAF yapandisha hadhi ya zawadi ya mshindi wa CHAN 2018

  (GMT+08:00) 2018-01-11 09:29:19
  Shirikisho la vyama vya soka barani Afrika CAF, limetangaza zawadi rasmi za washindi wa kombe la mataifa kwa wachezaji wa ndani CHAN litakazofanyika mwezi uajo nchini Morocco.

  Bingwa atajitwalia kombe pamoja na fedha taslimudola za kimarekani milioni 2.5, ikiwa ni ongezeko la asilimia 67 ikilinganishwa na zawadi ya mshindi wa mashindano yaliyopita ambayo ilikuwa dola 750,000.

  Ongezeko hilo limetokana na pesa zilizopatikana baada ya CAF kusaini mikataba mipya na wadhamini wa mashindano hayo ambao ni kampuni ya wauzaji mafuta ya Total.

  Mshindi wa pili atakabidhiwa dola 700,000, kwa kuingia nusu fainali ni dola 400,000, dola 300,000 kwa watakofika robo fainali na madau yote hayo ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimi 60 ikilinganishwa na mashindano yaliyopita.

  Lakini timu zote zinazoshiriki mwaka huu zitakabidhiwa fedha ya ushiriki dola 100,000.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako