• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Guniea ya Ikweta yasema uasi uliozimwa mwishoni mwezi uliopita yalipangwa nchini Ufaransa

    (GMT+08:00) 2018-01-11 20:15:26

    Waziri wa mambo ya nje wa Guniea ya Ikweta Bw. Agapito Mba Mokuy amesema uasi uliozimwa mwishoni mwa mwaka jana ulipangwa nchini Ufaransa lakini serikali ya Ufaransa haihusiki.

    Shirika la habari la Ufaransa lilimnukuu Bw. Mokuy akisema, nchi yake itashirikiana na Ufaransa kuanza uchunguzi baada ya kupata taarifa zaidi. Mpaka sasa wamluki 27 waliohusika na uasi huo wamekamatwa na wengine 150 wametoroka.

    Bw. Mokuy amesema, kutokana na uasi huo, na pia haijakuwa tayari kikamilifu, Guniea Ikweta imesimamisha kwa muda kujiunga na makubaliano ya mawasiliano ya watu ndani ya eneo la katikati ya Afrika yaliyopitishwa na jumuiya ya uchumi na sarafu ya eneo hilo mwezi Oktoba mwaka 2017.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako