• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa pili wa viongozi wa ushirikiano wa Lancang-Mekong watoa Azimio la Phnom Penh

  (GMT+08:00) 2018-01-11 20:36:42

  Mkutano wa pili wa viongozi wa ushirikiano wa Lancang-Mekong wenye kauli mbiu "Mto wa amani na maendeleo endelevu" umefanyika leo huko Phnom Penh, Cambodia.

  Mkutano huo umetoa azimio la Phnom Penh, na kuelekeza maendeleo ya miaka 10 ijayo ya mfumo wa ushirikiano huo. Azimio hilo linasema, mfumo huo umeendelezwa na kuwa mfumo pevu wa ushirikiano wa kikanda, na umehimiza maendeleo ya jamii na uchumi wa kikanda, na kuinua kiwango cha maisha ya watu. Pia umesaidia kupunguza tofauti ya maendeleo, kuunga mkono ujenzi wa jumuiya ya Asia Kusini Mashariki, kuhimiza ushirikiano wa Kusini na Kusini, na kusukuma mbele utekelezaji wa agenda ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030.

  Azimio hilo linasema mfumo huo utaimarisha zaidi ushirikiano katika pande tano zitakazopewa kipaumbele, kupanua ushirikiano mpya, kukabiliana na mahitaji ya maendeleo ya nchi za mto Lancang-Mekong, na kuboresha muundo wa ushirikiano na kujenga kwa pamoja ukanda wa maendeleo ya uchumi wa kanda hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako