• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaziunga mkono Korea Kaskazini na Korea Kusini kuhimiza mazungumzo kati yao

  (GMT+08:00) 2018-01-12 08:41:59

  Rais Xi Jinping wa China amesema China inaunga mkono kuboreshwa kwa uhusiano kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini, na inahimiza maafikiano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Akizungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Korea Kusini Bw. Moon Jae-in, rais Xi Jinping amesema China inaziunga mkono pande hizo mbili kuhimiza mazungumzo na mawasiliano kati yao, na kusukuma mbele hatua kwa hatua utatuzi wa suala la peninsula ya Korea. Rais Xi pia amesema China inapenda kuimarisha ushirikiano na pande zote husika, ikiwemo Korea Kusini, ili kuhimiza matokeo chanya kwenye maendeleo ya suala hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako