• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwenyekiti wa kamati ya umoja wa Afrika atoa mwito wa kuhimiza mapambano dhidi ya ufisadi barani Afrika

    (GMT+08:00) 2018-01-12 08:54:11

    Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Mahamat amehimiza mwito wa kuwepo kwa juhudi za pamoja kupambana na ufisadi barani Afrika.

    Taarifa iliyotolewa jana na mwenyekiti huyo inazitaka nchi wanachama wa umoja huo, jumuiya za uchumi za kikanda, idara za Umoja wa Afrika, mashirika yasiyo ya kiserikali, wananchi na wadau wengine, kufanya kazi pamoja katika mwaka huu, na baada ya mwaka huu, kuondoa mzigo wa ufisadi kwa waafrika wanaoathiriwa na tatizo hilo.

    Umoja wa Afrika umeutangaza mwaka huu kuwa ni mwaka wa kupambana na ufisadi.

    Mwito huo umetokea wakati umoja wa Afrika wenyewe umekuwa ukitafuta njia ya kujiendesha kwa fedha za kujitegemea. Maofisa wa mambo ya fedha wa umoja wa Afrika wanaokutana mjini Kigali, wamesema usimamizi mzuri na uwajibikaji kwenye mambo ya fedha, utafanya umoja wa Afrika uwe taasisi endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako