• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uhamiaji watajwa kuwa hali chanya duniani

    (GMT+08:00) 2018-01-12 10:00:19

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amezitaka serikali za nchi mbalimbali kuutambua uhamiaji kama hali chanya duniani, na kutoweka vizuizi dhidi ya uhamiaji halali wa kimataifa.

    Akiongea kwenye mkutano usio rasmi wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa unaoandaa makubaliano ya kimataifa kuhusu uhamiaji, Bw. Guterres amesema kuwa uhamiaji ni hali chanya duniani, ambayo inachochea ukuaji wa uchumi, na kupunguza hali isiyo ya haki, kuunganisha jamii tofauti na kupunguza matatizo ya kutokuwepo kwa uwiano kwenye idadi ya watu duniani.

    Amesema nchi mbalimbali zinahitaji kuimarisha utawala wa kisheria unaolenga kusimamia na kulinda wahamiaji, ili kuhakikisha maslahi yao ya kiuchumi, kuboresha mazingira ya kuishi na kuwanufaisha wahamiaji hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako