• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bondia Deontay Wilder apewa adhabu kwa kutokana na kosa la kutumia bangi

    (GMT+08:00) 2018-01-12 10:21:26
    Bingwa wa uzito wa juu wa WBC Deontay Wilder amehukumiwa kifungo cha kufanya kazi za kijamii kwa saa 60 kutokana na kukutwa na hatia ya kumiliki bangi.

    Askari wa barabarani mjini Tuscaloosa walikuta vipande vya bangi katika gari ya Wilder baada ya kulikaguwa kwenye msako wa kawaida.

    Judge Ricky McKinney alimwagiza bondia huyo mwenye miaka 32 kwenda kushiriki kazi ya kusafisha kituo cha kuendeleza vijana cha YCMA.

    Lakini wakili wa bondia huyo, alitetea kuwa, bangi hiyo haikuwa yake isipokuwa rafiki zake ambao walikuwa wakitumia gari hiyo alipokuwa safarini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako