• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaipinga Marekani kupitisha muswada kuhusu suala la Taiwan

  (GMT+08:00) 2018-01-12 14:12:27

  Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amesema, China inapinga kithabiti mswada uliopitishwa hivi karibuni kwenye baraza la chini la bunge la Marekani unaokiuka vikali sera ya kuwepo kwa China moja, na kanuni ya taarifa tatu za pamoja kati ya China na Marekani, na kuingilia kati mambo ya ndani ya China.

  Bw. Lu Kang amesisitiza kuwa China inaihimiza Marekani ifuate sera ya kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za pamoja, kushughulikia kwa makini suala la Taiwan, kutowasiliana na mamlaka ya Taiwan kwa njia yoyote ya kiserikali, kutotoa ishara yoyote ya makosa kwa nguvu inayojaribu kuifanya Taiwan ijitenge na China, na kulinda kwa hatua halisi uhusiano kati ya China na Marekani, na ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika mambo ya kimataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako