• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wakenya waishio Marekani wafurahishwa na safari za KQ za moja kwa moja Marekani

  (GMT+08:00) 2018-01-12 18:57:41

  Wakenya waishio Marekani wamefurahishwa na hatua ya shirika la ndege la Kenya Airways ya kuanzisha safari za moja kwa moja kutoka Nairobi hadi Marekani.Wakenya hao wamesema wamekuwa wakihangaishwa na mashirika makuu ya ndege duniani kwa kutakikana kuwa na viza za mataifa wanayopitia kabla ya kuwasili Marekani.Hatua hiyo itaokoa wakati na kuwafanya wakenya kutumia fedha kidogo za nauli ya ndege. Ndege za Trans-Atlantic zimeratibiwa kutoka uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta International Airport kuanzia saa nne usiku kisha kuwasili Marekani baada ya saa 15 kila siku. Hii ni kinyume na awali ambapo abiria walikuwa wanachukua muda wa saa 22 kupitia ulaya ndio wafike Marekani kutoka Nairobi. Tayari KQ imeanza kuuza tiketi za moja kwa moja hadi Marekani kwa wale wanaotaka kusafiri kuanzia Octoba 28 mwaka huu.Wakenya wanaoishi miji mbali mbali Marekani watatumia ndege za shirika la Delta ambalo lina mkataba wa usafiri na KQ kupitia shirika la KLM kupelekwa mjini New York.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako