• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Magufuli apokea taarifa ya umiliki wa kampuni ya simu ya Airtel

  (GMT+08:00) 2018-01-12 18:58:02

  Waziri wa Fedha na Mipango Bw.Philip Mpango amewasilisha taarifa ya kamati aliyoiunda kuchunguza umiliki wa Kampuni ya Simu ya Airtel kwa Rais John Pombe Magufuli, aliyeagiza kufanyika kwa uchunguzi huo Desemba 20, mwaka jana.

  Wakati huo huo Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amekamilisha Kanuni za Sheria ya Madini Namba 7 ya mwaka 2017 na kuwasilisha vitabu vya kanuni hizo kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi.

  Taarifa nyingine iliyowasilishwa kwa Rais ni ya utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Novemba 25, mwaka jana wakati wa ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi (Mloganzila) kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

  Akiwasilisha taarifa yake, Dk Mpango alisema Serikali imejiridhisha kuwa ubinafsishaji wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL) kwenda Celtel, baadaye kuhamishiwa Zain na sasa Airtel, ulifanyika kwa ukiukwaji mkubwa wa sheria, kanuni na taratibu. Kufuatia ukiukwaji huo, Dk Mpango alisema Serikali inayomiliki asilimia 40 ya hisa za kampuni ya Airtel, imeamua kufanya mazungumzo na kampuni ya Airtel inayomiliki asilimia 60 ya hisa ili nchi iweze kupata haki yake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako