• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani kuongeza kwa mara ya mwisho muda wa kusimamisha vikwazo dhidi ya Iran

    (GMT+08:00) 2018-01-13 17:23:08

    Rais Donald Trump wa Marekani ataongeza kwa mara ya mwisho muda wa kusimamisha vikwazo dhidi ya Iran kwa mujibu wa makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015.

    Kwa mujibu wa maofisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Marekani, rais Trump anatarajia kuyafanyia marekebisho makubwa makubaliano hayo ya kihistoria yaliyofikiwa mwezi Julai, mwaka 2015 kati ya Iran na nchi 6 za Marekani, Uingereza, Ufaransa, Russia, China na Ujerumani katika siku 120 zijazo, ama sivyo ataiagiza Marekani kujitoa kwenye Makubaliano hayo.

    Wakati rais Trump anaamua kuongeza muda wa kusimamisha vikwazo dhidi ya Iran, Wizara ya Fedha ya Marekani ilisema imeweka vikwazo dhidi ya watu na mashirika 14 kutokana na tuhuma za ukiukaji wa haki za binadamu na mpango wa makombora aina ya ballistic.

    Naye waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amesema tangazo hilo la rais Trump kuhusu makubaliano ya kimataifa kuhusu nyuklia ni jaribio la kukata tamaa na linakiuka vibaya vipengele katika makubalino hayo. Ameongeza kuwa makubaliano hayo hayapaswi kujadiliwa, na Marekani inapaswa kuyatekeleza kikamilifu kama Iran.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako