• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China aanza ziara yake barani Afrika

    (GMT+08:00) 2018-01-14 16:58:59

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema China iko tayari kuimarisha mawasiliano na Rwanda katika nyanja mbalimbali kutoka uongozi hadi utamaduni.

    Bw. Wang sasa yuko ziarani barani Afrika, ambako Rwanda ni kituo cha kwanza katika ziara hiyo. Jana alipokutana na rais Paul Kagame wa Rwanda, mjini Kigali, Bw. Wang alipongeza uhusiano mzuri kati ya nchi hizo mbili unaotokana na maelewano, kuaminiana na kuungana mkono kwa muda mrefu. Amesema Rwanda imejipatia njia ya maendeleo endelevu inayoungwa mkono na wananchi wake, na kwamba China inapenda kuimarisha mawasiliano na Rwanda katika uzoefu wa uongozi wa nchi na kuzidisha hali ya kuaminiana kisiasa.

    Kwa upande wake, rais Kagame alisema Afrika inaiamini China na inapenda kuona China ikifanya kazi muhimu zaidi barani humo. Ameishukuru China kutokana na uungaji mkono na mchango wake kwa maendeleo ya Rwanda.

    Wakati huohuo, kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya kukutana na rais Kagame, Bw. Wang amesema mawaziri wa mambo ya nje wa China wanaichukulia Afrika kuwa ya kwanza katika ziara ya kila mwaka, hii inaonesha kuwa Afrika siku zote ni kipaumbele cha diplomasia ya China. Amesema desturi hiyo imedumu kwa miaka 28 na China ni rafiki na mwenzi anayetegemewa zaidi na ndugu wa Afrika.

    Bw. Wang pia ameeleza matarajio ya nchi yake kuhusu mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika mjini Beijing mwaka huu, akisema FOCAC ni njia muhimu ya kufanya mazungumzo ya pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Afrika, na pia ni jukwaa kubwa na lenye matunda mengi zaidi kwa nchi 29 wanachama wa ushirikiano wa Kusini na Kusini. Amesema mkutano wa kilele wa FOCAC uliofanyika Johannesburg ulipata mafanikio makubwa na China inapenda kushirikiana na marafiki wa Afrika kufanya mkutano wa mwaka huu na kuupeleka kwenye ngazi ya juu zaidi. Amesema nchi nyingi za Afrika zinapongeza na kuunga mkono pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja lililotolewa na rais Xi Jinping na China inapenda kuingiza uhai mpya kwenye ushirikiano na Afrika kwa kupitia kujenga kwa pamoja pendekezo hilo.

    Baada ya kumaliza ziara yake nchini Rwanda, Bw. Wang aliendelea na ziara yake nchini Angola, ambapo alikutana na rais Joao Lourenco wa nchi hiyo mjini Luanda. Bw. Wang alisema China inaiunga mkono Angola katika kutafuta njia ya maendeleo inayolingana na hali ya nchi hiyo, kuhimiza mkakati anuwai wa uchumi na kuongeza uwezo wa kujiendeleza.

    Ameongeza kuwa China inapenda kuimarisha ushirikiano wa kivitendo na Angola, kuinua uhusiano wa pande mbili kwenye ngazi mpya na kupanua maeneo yatakayofanyiwa ushirikiano.

    Kwa upande wake, rais Lourenco alisema ushirikiano wa pande mbili umepata mafanikio mengi baada ya nchi hizo kuanzisha uhusiano wa kibalozi miaka 35 iliyopita. Ameishukuru China kutokana na uwekezaji na msaada wake wa kifedha, ambao umefanya kazi muhimu katika kujenga amani nchini Angola, ambako vita ilimalizika mwaka 2002 baada ya kudumu kwa miaka 27.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako