• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakanusha madai kuwa mikopo yake inaongeza mzigo kwa Afrika

    (GMT+08:00) 2018-01-15 10:45:05

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amekanusha madai yasiyo na msingi yanayosema mikopo ya China imeongeza mzigo wa madeni kwa nchi za Afrika.

    Bw. Wang ambaye yuko ziarani nchini Angola amesema hayo huko Luanda wakati akikutana na wanahabari, pamoja na mwenzake wa Angola Bw. Manuel Domingos Augusto. Amesema China inatoa mikopo kwa mujibu wa kanuni za kunufaishana, kulingana na mahitaji halisi ya Afrika na bila masharti yoyote ya kisiasa, na kwamba mzigo wa madeni kwa baadhi ya nchi za Afrika ni wa muda mrefu, na njia ya kutatua suala hilo ni kuleta maendeleo endelevu. Amesema China inapenda kuendelea kusaidia kuijengea Afrika uwezo wa kujiendeleza.

    Aidha, Bw. Wang amehimiza mageuzi na maboresho ya ushirikiano kati ya China na Angola, na kuutaja uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili kuwa mfano mzuri wa ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Afrika.

    Kwa upande wake Bw Augusto amesema Angola inathamini uhusiano kati yake na China, itaendelea kufuata sera ya kuwepo kwa China moja duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako