• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • PLO yajadili njia ya kukabiliana na uamuzi wa Marekani wa kutambua Jerusalem mji mkuu wa Israel

  (GMT+08:00) 2018-01-15 14:41:02

  Chama cha ukombozi cha Palestina PLO Jumapili kimeitisha mkutano kujadili mkakati mpya wa kukabiliana na hatua ya Marekani kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, licha ya kususiwa na makundi makubwa ya Palestina Hamas na Jihad.

  Mkutano huo ulioshirikisha kamati tendaji ya PLO na Baraza la Taifa la Palestina PNC, pia utajadili na kutathmini hatma ya mchakato wa amani uliokwama kati ya Palestina na Israel.

  Wakati wa mkutano huo wa siku mbili, mwanachama wa kamati kuu ya chama cha Fatah Bw. Jamal Muheisen amelihimiza baraza kuu la chama cha PLO kufuta uamuzi wa kuitambua Israel, akisema si busara kuendelea kuitambua Israel wakati ikiipinga Palestina na uongozi wake.

  Pia amesema viongozi wa Palestina wanapaswa kufanya upinzani kwa amani dhidi ya sera za Israel kwa watu wa Palestina na ardhi yao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako