Kenya imefufua mipango ya kujenga mtambo wake wa kwanza wa umeme wa gesi huko Mombasa baada ya kuacha mradi huo mwaka 2016.
Waziri wa kawi Charles Keter ameanzisha mazungumzo mapya na Hazina ya fedha katika kuandaa muundo wa fedha kwa kituo cha kuzalisha kawi cha megawatt 700 (MW) ambacho serikali inataka kutekeleza pamoja na mwekezaji binafsi chini ya mfano wa ushirika wa kibinafsi.
Mnamo mwaka wa 2016,wizara ya kawi ilisitisha mradi wa gesi asili mjini Mombasa, ambayo ilikadiriwa kugharamu sh bilioni 130.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |