• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chama cha Soka Ufaransa, chamsimamisha mwamuzi kwa uonevu

    (GMT+08:00) 2018-01-16 10:26:40
    Chama cha Soka cha Ufaransa kimetangaza kumsimamisha kazi kwa muda usiojulikana mwamuzi Tony Chapron aliyemrushia teke mchezaji wa klabu ya Nantes nchini Ufaransa Diego Carlos kabla ya kumuondoa uwanjani wakati wa mechi yao dhidi ya Paris St-Germain.

    Diego alimgonga mwamuzi kwenye kisigino katika kilichoonekana kama ajali tu dakika za mwisho za mechi.

    Lakini Chapron alimrushia teke mchezaji huyo na kisha akampa kadi ya pili ya njano, kwa sababu ya kulalamika.

    Katika mechi hiyo PSG walishinda kwa 1-0. Na tayari Chapron alikuwa ameteuliwa kusimamia mechi ya Ligue 1 kesho Jumatano kati ya Angers na Troyes. Nantes wanataka kadi hiyo ibatilishwe kwani isipobatilishwa kwani isipobatilishwa Diego atakosa mechi moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako