• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa EAC kujadili miundombinu ya afya na maendeleo mwezi ujao

    (GMT+08:00) 2018-01-16 20:50:41

    Mkutano wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), uliokuwa ufanyike Novemba mwaka jana, sasa umepangwa kufanyika Februari Kampala, Uganda.

    Mkutano huo unatarajiwa kuwa na uzito wa kipekee kutokana na viongozi wa EAC kujadili masuala ya miundombinu ndani ya nchi sita za EAC, afya na maendeleo yake kwa ujumla.

    Mbali ya waasisi wa jumuiya hiyo nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, wanachama wengine ni Rwanda, Burundi na Sudan Kusini. Kwa mujibu wa taarifa ya Sekretarieti ya EAC kwa umma, mkutano huo unatarajiwa kushirikisha wajumbe zaidi ya 1,000 wa ndani na nje ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

    Wanatarajiwa kuzama katika kujadili masuala la miundombinu, fedha za tiba na maendeleo kwa kutumia kaulimbiu 'Kukuza na Kupanua mtangamano kwenye miundombinu na maendeleo ya sekta ya afya nchi za EAC'.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako